Mwanaume kama una tabia ya kumnyanyasa mke wako, soma hapa ujifunze kitu

 

Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume.

Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikuwa karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhuduia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi.

Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na namuudhi. Kwasiku tatu zote nilikuwa karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikuwa wakimlilia Mama yao.

Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi? Wanamuuliza Bibi yao Mama yuko wapi? Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anambembeleza mdogo wake alikuwa anamuambia.

“Usilie Mama kaenda sehemu nzuri, kaenda kupumzika kwa Mungu na Malaika…” Mdogo wake ndipo alipouliza Baba nayeye, akasema “Amemsindikiza Mama watakaa huko na mimi ndiyo nitakulinda, usiogope nipo hapa. Unakumbuka siku ile Mama alivyotuambia twende kwa Bibi kukaa wenyewe…”

Alimuuliza… “Mimi si nilikulinda…nitakulinda na sasa…Mama ametuangalia lakini sisi hatumuoni….” Kama hapo umelia basi subiri majibu ya yule mdogo wake. Huku akijaribu kujizuia kulia alimuuliza Kaka yake. “Sasa kama Baba ameenda na Mama si atampiga tena, mimi sitaki Mama apigwe, kwanini asingeenda peke yake…

.” Nilianza kuwaza namna ambavyo rafiki yangu yule alikuwa akimnyanyasa mkewe, namna alivyokua akimpiga na kumsimanga, nilishaongea naye mara nyingi lakini hakujali.

Lakini alikuwa anawapenda watoto wake na kila siku aliwadekeza ila hawakumkumbuka. Jibu la kijana wake ndiyo lilinifanya niamini kuwa wanadamu si chochote. “Huko hawezi kumpiga, Mama ameenda kwa Mungu, huyo ana nguvu zaidi kuliko Baba. Akimsogelea tu Mama atamchanachana kama karatasi! Mungu ana upendo hapigi watu wema kama Mama!”

Hapo yule mtoto alikuwa akiongea kwa uchungu lakini kwa hasira na kwa imani kabisa. Sikuweza kuendelea kuvumilia kuwasikiliza, niliwaacha na kwenda kumuangalia mke wangu, nilimkumbatia na kumuuliza “Mke wangu hivi na mimi nakunyanyasa?”

Aliniangalia kwa mshangao, aliniulzia kwanini unasema hivyo, nilimuambia hapana niambie tu. Niambie kama kuna kitu nakifanya kinakukwaza ambacho watoto wangu watakiona. Nilimuambia “Nataka wanangu waniulizie nikifa, sitaki wanangu wafurahie kifo changu.

” Mke wangu alinikumbatia huku akitokwa na machozi aliniambia “Hakuna mume wangu, wewe ni mume bora, sema uache tu kuweka soksi kwenye makochi na kuacha sahani Kitandani.”

Nilijikuta natabasmau kidogo, kwani mke wangu alikuwa na furaha. Sasa hivi najifunza nisiache soksi kwenye makochi wala sahani kitandani. Najua alikua anatania ila kama kinamkera nitaacha, maisha hapa duniani ni mafupi, watoto ndiyo kitu tunaacha kwaajili ya kututambulisha, sitaki wanangu wanaitambue kama Baba mkatili. Hupati faida yoyote kwa kumnyanyasa mke wako na wala haikufanyi kuwa mwanaume zaidi!

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE JIFUNZE JINSI YA KUKATA KIUNO KITANDANI KAMA FENI NA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO KWA KIUNO LAINI

Bado ulaji wa vyakula mbali mbali kitaifa ni tatizo- Waziri Hasunga