Mariam Ditopile awakumbusha wanawake na vijana jinsi Magufuli alivyowainua

 

MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amesema miaka mitano ya serikali ya Dk John Magufuli imekua ya manufaa makubwa kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Amesema makundi hayo yamenufaika kwa kiasi kikubwa na serikali ya Magufuli kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri zote nchini.

Mikopo hiyo imekua inatolewa kwa vikundi kwa ajili ya biashara mbalimbali na faida yake ni kwamba ni ile mikopo isiyo ya ribs jambo ambalo limekua na manufaa makubwa kwa wananchi wa maisha ya chini.

" Leo tunapoomba kura ndugu zangu tunataja mambo kama haya ambayo Rais Magufuli ameyafanya kwa miaka mitano, hizi fedha zinazotolewa na Halmashauri siyo mikopo ni kama umeazimwa tu maana hakuna cha riba.

Wanaosema Magufuli anafanya maendeleo ya vitu tunapaswa tuwaambie jinsi ambavyo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu walivyonufaika na fedha hizi, hapa Dodoma kuna vijana walianza na mkopo wa Milioni mbili lakini leo wanakaribia kuchukua Milioni 15 na wameshapiga hatua kubwa kimaendeleo," Amesema Ditopile.

Akizungumza kwenye kampeni kata ya Makole jijini Dodoma, Ditopile amewaomba vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kumuunga mkono mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli ili aweze kumalizia kazi ya kuwatumikia watanzania ambayo alishaianza.

" Tusijaribu sumu kwa kuilamba, miaka mitano tulimuamini Magufuli atufanyie kazi na kweli ameifanya, vijana na wanawake mmenufaika sana na mpango wake we kuwainua kupitia hizi fedha za Halmashauri, mpeni kura nyingi ili aweze kututumikia tena," Amesema Ditopile.

 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE JIFUNZE JINSI YA KUKATA KIUNO KITANDANI KAMA FENI NA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO KWA KIUNO LAINI

Bado ulaji wa vyakula mbali mbali kitaifa ni tatizo- Waziri Hasunga