NASA yatangaza mpango wa kuwapeleka wanaanga mwezini

 


Shirika la anga za mbali la Marekani, NASA, limetangaza mpango wa kutuma tena wanaanga mwezini, kwa gharama ya takribani dola bilioni 28. Kati ya hizo, chombo cha kuwapeleka wanaanga hao kitagharimu dola bilioni 16. 

Mpango huo ulianzishwa na rais Donald Trump kama mojawapo ya vipaumbele vya utawala wake, utahitaji idhini ya bunge la nchi hiyo linalokabiliwa na uchaguzi wa mwezi Novemba. 

Gharama hiyo ya Dola bilioni 28 inapaswa kupatikana katika bajeti ya miaka minne kati ya 2021 na 2025. 

Katika mazungumzo na waandishi wa habari, mkuu wa NASA Jim Bridenstine amesema hofu za kisiasa ni changamoto kubwa kwa kazi ya shirika lake. 

Rais wa zamani Barack Obama aliufuta mradi wa kupeleka wanaanga katika sayari ya Mars, baada ya mtangulizi wake kutumia mabilioni ya dola kuuandaa.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE JIFUNZE JINSI YA KUKATA KIUNO KITANDANI KAMA FENI NA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO KWA KIUNO LAINI

Bado ulaji wa vyakula mbali mbali kitaifa ni tatizo- Waziri Hasunga