Posts

Showing posts from September, 2020

NASA yatangaza mpango wa kuwapeleka wanaanga mwezini

Image
  Shirika la anga za mbali la Marekani, NASA, limetangaza mpango wa kutuma tena wanaanga mwezini, kwa gharama ya takribani dola bilioni 28. Kati ya hizo, chombo cha kuwapeleka wanaanga hao kitagharimu dola bilioni 16.  Mpango huo ulianzishwa na rais Donald Trump kama mojawapo ya vipaumbele vya utawala wake, utahitaji idhini ya bunge la nchi hiyo linalokabiliwa na uchaguzi wa mwezi Novemba.  Gharama hiyo ya Dola bilioni 28 inapaswa kupatikana katika bajeti ya miaka minne kati ya 2021 na 2025.  Katika mazungumzo na waandishi wa habari, mkuu wa NASA Jim Bridenstine amesema hofu za kisiasa ni changamoto kubwa kwa kazi ya shirika lake.  Rais wa zamani Barack Obama aliufuta mradi wa kupeleka wanaanga katika sayari ya Mars, baada ya mtangulizi wake kutumia mabilioni ya dola kuuandaa.

Mariam Ditopile awakumbusha wanawake na vijana jinsi Magufuli alivyowainua

Image
  MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amesema miaka mitano ya serikali ya Dk John Magufuli imekua ya manufaa makubwa kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu. Amesema makundi hayo yamenufaika kwa kiasi kikubwa na serikali ya Magufuli kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri zote nchini. Mikopo hiyo imekua inatolewa kwa vikundi kwa ajili ya biashara mbalimbali na faida yake ni kwamba ni ile mikopo isiyo ya ribs jambo ambalo limekua na manufaa makubwa kwa wananchi wa maisha ya chini. " Leo tunapoomba kura ndugu zangu tunataja mambo kama haya ambayo Rais Magufuli ameyafanya kwa miaka mitano, hizi fedha zinazotolewa na Halmashauri siyo mikopo ni kama umeazimwa tu maana hakuna cha riba. Wanaosema Magufuli anafanya maendeleo ya vitu tunapaswa tuwaambie jinsi ambavyo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu walivyonufaika na fedha hizi, hapa Dodoma kuna vijana walianza na mkopo wa Milioni mbili lakini leo wanakaribia kuchukua Milioni 15 na wamesha

Tanzania na Ujerumani kuendeleza ushirikiano kuimarisha Sekta ya Elimu

Image
  Serikalini ya Tanzania na Ujerumani wamekubalina kuendeleza mashirikiano kwenye elimu  ya juu, Ufundi na Msingi ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata ujuzi wa kuweza kushiriki katika ujenzi wa Taifa.  Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wawakilishi kutoka ubalozi wa Ujerumani na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kilichofanyika katika Ofisi za wizara Jijini Dodoma Katibu Mkuu Dkt Leonard Akwilapo amesema kwa sasa nchi inatekeleza miradi  mikubwa ya ujenzi hivyo kuna  uhitaji wa wataalamu wenye ujuzi katika eneo. “Tunajenga reli ya kisasa ya umeme SGR, madaraja na ipo miradi mingine mikubwa inatekelezwa, pamoja na kwamba tunao wataalamu wetu nchini bado tunahitaji wajiendeleze ili kupata ujuzi zaidi. Kwa hiyo tumezungumza nao kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kuwezesha mafunzo  kwa Vijana  hapa nchini na hata nchini kwao,” aliongeza Dkt. Akwilapo. Akizungumzia uimarishaji wa elimu ya Msingi Katibu Mkuu Akwilapo amesema wamekubaliana kushirikiana  kuongeza u