Sweden waandamana kukemea mauaji ya George Floyd

Maandamano kukemea mauaji ya mmarekani mweusi  Gerorge Floyd yazidi kuvuka mipaka.

Maandamano ya kukemea mauaji ya mmarekani mweusi aliokufa mikononi mwa maafisa wa jeshi la Polisi Marekani yazidi kuvuka mipaka.

George Floyd alifariki baada ya kukandamizwa shingoni na goti la afisa alieonekana katika video iliorikodiwa kwa simu na kurushwa moja kwa moja kupitia mitandoa ya kijamii.

Baada ya kitendo hicho cha kulaaniwa maandamano yalianzia  mjini Minneapolis na kuenea katika mii takriban yote nchini Marekani.

Maandamano hayakukomea hapo , yamevuka mipaka hadi katika mataifa ya bara la Ulaya  na Argentina.

Maandamano ya kukemea mauaji hayo na matumizi ya nguvu ya kukithiri ya maafisa wa Polisi yamefanyika katika mataifa tofauti ikiwemo nchini Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Sweden.

Waandamanaji katika eneo la Segel Torg  nchini Sweden wamekemea mauaji hayo na kukemea ubaguzi wa rangi wakitumia neno la mwisho la George Floyd akiwa hao "Siwezi kupumua".

Jeshi la Polisi limesema kuwa limekabiliana na waandamanaji baada ya kuonekana kwamba masharti yaliwekwa kwa ajili ya kuepuka maambukizi ya virusi vya corona hayaheshimiki katika maandamano, jeshi la Polisi lililazimika kutumia mabomu ya kusababisha kutokwa na machozi kwa lengo la kuwasambaratisha na kuepuka maambukizi.

Mats Erickson, msemaji wa  jeshi la Polisi mjini Stockholm  amesema kwamba baadhi ya watu waliohusika na  wito wa mkusanyiko huo wamekamatwa.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE JIFUNZE JINSI YA KUKATA KIUNO KITANDANI KAMA FENI NA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO KWA KIUNO LAINI

Bado ulaji wa vyakula mbali mbali kitaifa ni tatizo- Waziri Hasunga