Sweden waandamana kukemea mauaji ya George Floyd
Maandamano kukemea mauaji ya mmarekani mweusi Gerorge Floyd yazidi kuvuka mipaka. Maandamano ya kukemea mauaji ya mmarekani mweusi aliokufa mikononi mwa maafisa wa jeshi la Polisi Marekani yazidi kuvuka mipaka. George Floyd alifariki baada ya kukandamizwa shingoni na goti la afisa alieonekana katika video iliorikodiwa kwa simu na kurushwa moja kwa moja kupitia mitandoa ya kijamii. Baada ya kitendo hicho cha kulaaniwa maandamano yalianzia mjini Minneapolis na kuenea katika mii takriban yote nchini Marekani. Maandamano hayakukomea hapo , yamevuka mipaka hadi katika mataifa ya bara la Ulaya na Argentina. Maandamano ya kukemea mauaji hayo na matumizi ya nguvu ya kukithiri ya maafisa wa Polisi yamefanyika katika mataifa tofauti ikiwemo nchini Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Sweden. Waandamanaji katika eneo la Segel Torg nchini Sweden wamekemea mauaji hayo na kukemea ubaguzi wa rangi wakitumia neno la mwisho la George Floyd akiwa hao "Siwezi kupumua". Jeshi l...