Serikalini ya Tanzania na Ujerumani wamekubalina kuendeleza mashirikiano kwenye elimu ya juu, Ufundi na Msingi ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata ujuzi wa kuweza kushiriki katika ujenzi wa Taifa. Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wawakilishi kutoka ubalozi wa Ujerumani na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kilichofanyika katika Ofisi za wizara Jijini Dodoma Katibu Mkuu Dkt Leonard Akwilapo amesema kwa sasa nchi inatekeleza miradi mikubwa ya ujenzi hivyo kuna uhitaji wa wataalamu wenye ujuzi katika eneo. “Tunajenga reli ya kisasa ya umeme SGR, madaraja na ipo miradi mingine mikubwa inatekelezwa, pamoja na kwamba tunao wataalamu wetu nchini bado tunahitaji wajiendeleze ili kupata ujuzi zaidi. Kwa hiyo tumezungumza nao kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kuwezesha mafunzo kwa Vijana hapa nchini na hata nchini kwao,” aliongeza Dkt. Akwilapo. Akizungumzia uimarishaji wa elimu ya Msingi Katibu Mkuu Akwilapo amesema wame...
Comments
Post a Comment