Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume. Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikuwa karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhuduia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi. Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na namuudhi. Kwasiku tatu zote nilikuwa karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikuwa wakimlilia Mama yao. Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi? Wanamuuliza Bibi yao Mama yuko wapi? Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anambembeleza mdogo wake alikuwa anamuambia. “Usilie Mama kaenda sehemu nzuri, kaenda kupumzika kwa Mungu na Malaika…” Mdogo wake ndip...